Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaa (DUCE) ni Chuo Kishiriki cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kilichopo makutano ya Barabara ya Taifa na Chang’ombe katika Kitalu Na.324 na 325 Karibu na Uwanja wa Mkapa (Zamani Uwanja Mkuu wa Taifa). Chuo chetu kinatarajia kuanza kufanya ukarabati wa majengo na miundombinu mbalimbali ndani ya Chuo. Hivyo, Chuo kinakaribisha maombi kutoka kwa mafundi wa fani mbalimbali kwa ajili ya utekelezaji wa kazi hizo kwa kuzingatia maelekezo kama yalivyobainishwa katika Barua iliyoambatanishwa hapo chini.
UTARATIBU WA KUTUMA MAOMBI YA ZABUNI
- Maombi yanayobainisha gharama za ufundi na viambatisho vinavyotakiwa viwekwe kwenye bahasha moja na juu ya bahasha paandikwe KATIBU WA BODI YA ZABUNI, (Taja eneo, kazi ama jengo unaloomba)
- Mwombaji anayetaka kuomba zaidi ya eneo moja atapaswa kuwasilisha barua zaidi ya moja akionesha maeneo anayoomba.
- Nyaraka kwa kila kazi itapatikana kwa gharama ya Shilingi elfu ishirini (Shilingi 20,000.00) katika Ofisi za Kitengo cha Kusimamia Manunuzi cha Chuo zilizoko karibu na Jengo jirani na lango kuu namba mbili la kuingilia Chuoni, kuanzia tarehe 13 Oktoba, 2020 muda ni saa mbili (2:00) asubuhi hadi saa tisa na nusu (9:30) alasiri kwa siku za kazi.
- Mwisho wa kupokea maombi haya ni tarehe 20 Oktoba, 2020 siku ya Jumanne saa sita na nusu (6:30) mchana ambapo itafuatiwa na zoezi la ufunguzi wa nyaraka hizo.
- Waombaji wote mnakumbushwa kuwepo siku ya ufunguzi.
- Maombi yote yawasilishwe moja kwa moja Chuoni DUCE. Chuo hiki kipo Mkabala na Uwanja wa Mkapa (Zamani Uwanja Mkuu wa Taifa).
- Mwombaji ataarifiwa kupitia namba yake ya simu na barua kwa anuani ya Posta aliyowasilisha endapo amefanikiwa kupata kazi baada ya tathmini kukamilika.
TAFADHALI PAKUA TAARIFA YA KINA KUHUSU SIFA NA TARATIBU ZA KUWASILISHA MAOMBI.