Naibu Rasi (Mipango, Fedha na Utawala) wa Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) anapenda kuwataarifu waombaji kazi mbalimbali waliofanya usaili tarehe 14 Septemba, 2022 hadi tarehe 19 Septemba, 2022 kuwa matokeo ya waombaji kazi waliofaulu usaili huo ni kama yalivyoorodheshwa katika tangazo hili. Waombaji waliofaulu usaili watatakiwa kukamilisha taratibu mbalimbali za ajira kuanzia tarehe 06 hadi 08 Oktoba, 2022 kwa kufika Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE). Aidha, waombaji kazi waliofaulu usaili wanatakiwa kuripoti katika Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) kuanzia saa sita mchana kwa tarehe 06 Oktoba 2022 na kuanzia saa tatu asubuhi kwa tarehe 07 Oktoba 2022 hadi 08 Oktoba 2022 wakiwa na nyaraka zilizoainishwa katika tangazo hili ili zihakikiwe na mwajiri kabla ya kupewa barua ya ajira. Kwa wale ambao majina yao hayapo katika tangazo hili watambue kuwa hawakupata nafasi/hawakufaulu usaili, hivyo wasisite kuomba kwa mara nyingine pindi nafasi za kazi zitapotangazwa. Nyaraka tajwa ni kama ifuatavyo: (i) Vyeti halisi (Original Certificates) na nakala za vyeti hivyo zilizothibitishwa na Mamlaka za kisheria (certified by Advocate/Magistrate) vya masomo kuanzia kidato cha nne na kuendelea; (ii) Cheti cha kuzaliwa; (iii) Nakala/namba ya Kitambulisho cha Tafia (NIDA); (iv) Picha ndogo tatu za rangi (three coloured passport size photographs
Kwa maelezo zaidi tafadhali pakua kiambatanisho hapo chini