Na Tumaini Kibangara, CMU
Katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake kwa mwaka 2025, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kimeadhimisha siku hii kwa kutekeleza jukumu lake la kuhudumia jamii kwa kutoa misaada kwa makundi yenye uhitaji.