Body
UFAFANUZI: MITIHANI MAALUM NA MITIHANI YA MARUDIO HAIJAFUTWA
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kimebaini taarifa zinazosambaa katika mitandao ya kijamii zikidai kuwa mitihani maalum na mitihani ya marudio imefutwa Chuoni. UDSM inapenda kuutaarifu umma, hususan wanafunzi, kwamba taarifa hizo si za kweli.
Mitihani maalum na mitihani ya marudio bado ipo na itaendelea kutolewa. Kilichobadilika ni wakati wa kuifanya. Ili kuongeza ufanisi wa kitaaluma mitihani hiyo sasa itafanyika ndani ya Kalenda ya kawaida ya kitaaluma ya Chuo. Mabadiliko haya hayaathiri viwango vya mitihani wala kubadilisha vigezo vya kuendelea na masomo.
Announcement Date