Body
FURSA ZA UFADHILI WA MASOMO NCHINI SAUDI ARABIA KWA MWAKA WA MASOMO 2025/2026
- Tunapenda kuwatangazia Watanzania kuwa Serikali ya Saudi Arabia imetoa fursa za Ufadhili wa masomo ya juu jumla ya nafasi mia moja na ishrini na saba (127) kwa Tanzania. Nafasi hizo ni kwa ngazi mbali mbali za vyuo vilivyopo nchini Saudi Arabia. Maombi ya Ufadhili wa masomo hayo yafanyike kupitia Wizara ya Elimu ya Saudi Arabia kwa kutumia linki ya https://studyinsaudi.moe.gov.sa
- Taarifa zaidi kuhusu vigezo vya muombaji (admission requirements), utaratibu wa kufanya maombi (Admission procedures), fani za kujiunga (programmes for admission) na maeneo yatakayo gharamiwa na ufadhili (scholarship benefits) zinapatikana kwenye linki hapo juu.
- Tunawashukuru
Announcement Date