Skip to main content
Body

TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI


Naibu Makamu Mkuu wa Chuo, Taaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam anapenda kuwataarifu waombaji kazi wote walioomba nafasi mbalimbali za ajira katika chuo hiki kuwa, usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 8 Machi 2025. Baada ya usaili, waombaji watakaofaulu watapangiwa vituo vya kazi. Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-

  1. Usaili utafanyika kuanzia tarehe kama ilivyooneshwa kwenye tangazo hili muda na sehemu ambapousaili utafanyika umeainishwa kwa kila Kada.
  2. Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi;
  3. Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpiga kura,Kitambulisho cha kazi, Kitambulisho cha Uraia au Hati ya kusafiria.
  4. Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha kuzaliwa, kidato cha IV, VI, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za Mwombaji.
  5. Wasailiwa watakaowasilisha Testimonials, Provisional Results, Statement of results, hati za matokeo za kidato cha IV na VI (form V and form VI results slips) HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI.
  6. Kila msailiwa atajigharamia kwa Chakula, Usafiri na Malazi.
  7. Kila Msailiwa azingatie tarehe, muda na mahali alipopangiwa kufanyia usaili.
  8. Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (kama TCU, NACTE au NECTA)
  9. Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi vigezo. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji ya tangazo husika.
  10. Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi zao za Kitaaluma wanapaswa kuja na vyeti vyao Halisi vya Usajili pamoja na Leseni za kufanyia kazi.
  11. Wasailiwa wote walioitwa kwenye usaili wahakikishe wanaingia kwenye akaunti zao na kunakili namba
    ya mtihani kwa kuwa namba hizo hazitatolewa siku ya usaili

    RATIBA YA USAILI WA MCHUJO

Announcement Date