UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM
INSTITUTE OF KISWAHILI STUDIES (IKS)

VISA NA MIKASA YA KESI MAARUFU DUNIANI NA KUKUMU ZAKE

Visa na mikasa ya kesi maarufu duniani na hukumu zake ni moja ya vitabu vinavyochapishwa kwa awamu. Vitabu hivyo vitakuwa na mkusanyiko wa kesi mbalimbalizilizowahi kutokea katika nchi mbalimbali na kuvuta hisia za watu wengi. Katika kitabu hiki ambacho ni toleo la kwanza, kuna kesi nyingi za mauaji ambazo nyingi kati ya hizo zinahusiana na masuala ya mapenzi na mahusiano pamoja na sababu nyingine za kibinadamu. Zipo kesi za mauaji zilizosababishwa na malezi ya watoto wetu kutokana na mkengeuko wa mahusiano ya kingono na mitandao ya kijamii.

Zipo kesi nyingi ambazo zinatufumbua macho kuhusu jinsi upelelezi wa kesi mbalimbali unavyoweza kufanywa kwa umahiri mkubwa na hatimaye wahusika kukamatwa, kushtakiwa na kutiwa hatiani. Wakati mwingine mtu anayeza kupanga kufanya uhalifu kwa umakini mkubwa akidhani kwamba hataweza kukamatwa, lakini alama moja inayoweza kuachwa na mhusika huyo ni chanzo kizuri kinachoweza  kusaidia kukamatwa kwake. Teknolojia hivi sasa imerahisisha kukamatwa kwa wahalifu wengi wa mauaji tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma.

Kitabu hiki kimeandikwa kwa lugha nyepesi na kitasaidia sana kuelimisha jamii kuhusu masuala mbalimbali ya uhalifu na hukumu zake. Hivyo basi, hata kama mtu ana lengo la kufanya uhalifu atambue kwamba, kwa namna yoyote ile atabainika na kukamatwa.

Bwana Shaban Kaluse ambaye ndiye mwandishi wa kitabu hiki anaamini kuwa, jamii utajifunza mengi kupitia simulizi za kesi hizi zilizomo katika kitabu hiki cha Toleo la kwanza.