UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM
INSTITUTE OF KISWAHILI STUDIES (IKS)

SEMI

MAANA NA MATUMIZI

Athumani B. Mauya alizaliwa mwaka 1950 katika kijiji cha Chigamba Kwa Makocho, kata ya Miono, Wilaya ya Bagamoyo. Alipata elimu ya msingi katika kijiji cha Kimange, wilaya ya Bagamoyo mwaka 1962 – 1965. Mwaka 1966 – 1968 alihudhuria shule ya kati Kikaro, Bagamoyo na hatimaye masomo ya Sekondari kidato cha I-IV Minaki mwaka 1969 – 1972 na V-VI Moshi mwaka 1973 – 1974. Kati yam waka 1975 – 1976 alitumikia Jeshi la Kujenga Taifa kabla ya kujiunga na Mafunzo ya Ualimu (Fizikia na Hisabati) katika Chuo cha Ualimu Kleruu.

Mwaka 1977 aliajiriwa na Wizara ya Elimu na kufundisha katika Shule ya Sekondari Nyakato, Bukoba hadi Februari 1979; Sekondaria ya Minaki hadi 1980 alipojiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kuhitimu Shahada ya Ualimu.

Mwaka 1983 alijiunga na Taasisi ya Elimu ya watu wazima ambko anafanya kazi hadi alipostaafu, akiwa mkufunzi na Mkuu wa Idara Elimu kwa Njia ya Posta. Amewahi kuhudhuria Mafunzo ya Elimu kwa njia ya Posta, ngazi ya cheti, Chuo Kikuu cha Londaon, Uingereza mwaka 1986. Pia amepata kuandika Makala mbalimbali za Kiswahili kaika magazeti ya Majira na Mzalendo kati ya mwaka 1992 – 2004.