Hili ni toleo la tatu la kamusi ya Kiswahili sanifu. Toleo la kwanza lilitolewa mwaka 1981. Toleo hilo lilikuwa kamusi ua kwanza ya maneno sanifu ya Kiswahili. Toleo lililofuata lilichaposhwa mwaka 2004. Oxford University press ndiyo mchapishaji wa matoleo yote matatu.
Uandishi wa toleo hili ni ushirikiano wa wanaleksikografia na wataalamu wa lugha na fasihi wa taasisi ya taaluma za Kiswahili (TATAKI) ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam ( ambayo zamani ilijulikana TUKI)
Mbali na hao, wataalam wengine, wadau na wapenzi mbalimbali, ndani na nje ya Afrika Mashariki, wameshiriki katika kutoa maoni yao juu ya namna ya kuliboresha toleo hili la tatu la kamusi ya Kiswahili sanifu.
Nakala Zaidi ya milioni 2 zimeuzwa hadi sasaa
Kamusi hii ina historia ndefu. Ni miaka Zaidi ya 45 toka wazo la kuibuni, kuitunga, kuitafiti, kuichapa chapisho la kwanza, kuihakiki , kuidurusu, kuipanua, kuisanifu upya na kuiboresha.
Kamusi hii imewashughulisha watu wengi kwa miaka mingi katika kuitunga na kuiendeleza. Kwa kuidurusu utapata thibitisho tosha la kukua na kwenda kwake na wakati
Toleo hili la tatu lililoboreshwa lina :
KAMUSI INAYOAMINIKA KOTE DUNIANI: ISOME. IHAKIKI. ITUMIE.