UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM
INSTITUTE OF KISWAHILI STUDIES (IKS)

KAMUSI SANIFU YA KOMPYUTA

Bw. Omari M. Kiputiputi ni mhitimu wa shahada mbili za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam: shahada ya BSC (Ualimu) 1979, na shahada ya MBA (Masoko) 2000.

 

Mwaka 1987, Bw. Kiputiputi na Dkt. Uiso wa Idara ya Fizikia, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, walitafsiri kwa Kiswahili kitabu kinachojulikana sana kwa wanafizikia cha Ordinary level Physics kilichoandikwa na A.F.Abbot. Bw. Kiputiputi pia aliwahi kushiriki katika jopo la kiufundi lililohariri mswada wa Kamusi ya Primary Technical Dictionary iliyotungwa na Prof. Rajmund Ohly na kuchapwa na IPI mwaka 1987. Aidha alishiriki katika jopo la uhariri wa Kamusi Sanifu ya Biolojia, Fizikia na Kemia, iliyochapishwa na TUKI mwaka 1990.

 

 Kutokana na mchango wake mkubwa katika kuendeleza lugha ya Kiswahili, mwaka 2000 Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) lilimtunukia Bw. Kiputiputi tuzo ya dhahabu ya Shaaban Robert. Mwaka 2010 alichaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa BAKITA kwa kipindi cha miaka mitatu; wadhifa ambao anaendelea nao hadi tunaandika taarifa hii.

 

Kamusi sanifu ya kompyuta imefungua mlango wa kuingizia teknolojia ya kompyuta katika Kiswahili. Ni kielelezo Dhahiri kwamba tukitimiza wajibu wetu itawezekana kufikisha maarifa ya kompyuta kwa walengwa kwa kutumia lugha yetu.

 

Hashim M. Twaakiyondo(PhD)

Mkurugenzi, Kituo cha Elimu  kwa Njia ya Kompyuta, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.