UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM
INSTITUTE OF KISWAHILI STUDIES (IKS)

FASIHI YA KISWAHILI : Utafiti na Maendeleo yake

Chapisho hili ni zao la ushirikiano kati ya Taasisi ya Taaluma za Kiswahili (TATAKI) na Chama cha Kiswahili Afrika Mashariki (CHAKAMA). Sura zilizomo katika chapisho hili zimetokana na Kongamano la CHAKAMA lililofanyika katika Chuo Kikuu cha Mount Kenya mjini Thika (Kenya)  mwaka 2015. Kongamano hilo lilihudhuriwa jna wajumbe kutoka maeneo mbaimbili duniani. Katika kongamano hili yaliibuka mambo mengi na muhimu kuhusu lugha ya Kiswahili na mustakabali wake ndani na nje ya Afrika mashariki. Kwa kuzingatia mwitikio wa hali ya juu wa washiriki wa kongamano na mada zilizowasilishwa katika kongamano hili waharirir waliona kuwa litakuwa jambo la welekevu kutoa vitabu viwili ambavyo ni Lugha ya Kiswahili: utafiti na maendeleo na Fasihi ya Kiswahili: utaditi na maendeleo. Toleo hili litawafaidisha wanataaluma wa ngazi mbalimbali kususani wahadhiri, wakufunzi na hata wapenzi na wasomaji wote wa Kiswahili. Hivyo tunawaalika wasomaji wetu na wapenzi wa lugha adhimu ya Kiswahili kusoma sura zilizomo katika toleo hili, kutafakri, kukosoa na kuboresha yaliyomo kwa manufaa ya maendeleo ya lugha hii na taaluma yake.

YALIYOMO:

 1. Changamoto za Kiteknohama katika ufundishaji wa Riwaya ya Kiswahili katika shule za upili nchini kenya.  (Anthony Oloo Owino, Kenneth Inyani Simba na Choge Susan).
 2. Mbinu ya kuvuta makini ya mtoto katika fasihi wa watoto. (L.H.Bakize)
 3. Uadilishaji wa Mtoto katika ujenzi wa jamii asili: Tathmini ya hadithi za Watoto.(Simon Ekiru)
 4. Jukumu la vyombo vya kielectroniki katika ukuzaji wa Fasihi ya watoto. (Herriet K. Ibala)
 5. Hatua za maendeleo ya utafiti katika fasihi ya watoto nchini Kenya. (Pamela M.Y. Ngugi)
 6. Riwaya ya kihistoria ya watoto: dafina iliyopuuzwa katika fasihi ya Kiswahili. (L.H.Bakize)
 7. Ulinganishaji wa simukizi za watunwa za Afrika na Amerika: mkabala wa tofauti za kijamii. (Grace Henry)
 8. Methali katika jamii ya wanandi: Chimbuko na uainishaji wake. (Naomi C. Jescah na Biwott K. Anthony)
 9. Methali za Kiswahili na utandawazi. (S. M. Obuchi na Kenyani Nabeta Sangili)
 10. Utafiti katika methali za Kiswahili. (Joseph Nyehita Maitaria)
 11. Fasihi tafsiriwa za kigeni: urafiki au uadui kwa fasihi ya Kiswahili. (Joseph Nyahita Maitaria, Prter M. Kinyanjui na Lea Mwangi)
 12. Uhakiki kiulinganisi ya matumizi ya lugha katika tafsiri ya Things Fall apart: shujaa Okinkwo. (Mosol Kandagor na Sophia Ali)
 13. Utandawazi na hejimonia: mfano katika riwaya za Kiswahili. (Gladya Kinara na Japheth Peter Muindu)
 14. Nyuso za utandawazi katika fasihi ya Kiswahili nchini Kenya. (Mikhail Gromov)
 15. Fasihi andishi ya Kiswahili na swala la dini: mifumo ya riwaya  ya Said Ahmed Mohamed na Euphrase  Kezilahabi. (Miriam Osore)
 16. Utadhmini wa itikadi katika riwaya za awali za S.A. Mohamed. (Murithi Joseph Jesee)
 17. Usetaji wa Tenzi katika riwaya za Kisasa: utenzi wa Mwanakupona na Takhmisa ya Liyongo. (Ombito Elizabeth Khalili)
 18. Mabadiliko ya mwanasiasa wa Afrika kwa mujibu wa ushairi wa Kiswahili. (Timothy Kinoti , M.Ngaruthi na Mwenda  Mukuthuria)
 19. Urazinishaji wa Mwafrika: Tafakuri ya drama ya Kiswahili. (Collins Kenga Munbo)
 20. Sanaa za maonyesho na fasihi ya Kiswahili. (Wanyenya Willy)
 21. Utenzi wa Mwanamiti. (Elizabeth Ombito Khalili)
 22. Mwacha Kwao Mfitini. (Yusuf Wambugu)