UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM
RESEARCH AND EDUCATION FOR DEMOCRACY IN TANZANIA (REDET)

Announcements

Tume ya Taifa ya Uchaguzi inawatangazia wananchi wote wa mikoa ya Dodoma (Dodoma CC, Bahi DC, Chamwino DC, na Kongwa DC) na Mbeya (Mbeya CC, Busokelo DC, Buchosa DC, Kyela DC, Mbeya DC) kuwa Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa kutumia Teknolojia ya “Biometric Voters Registration”utaanza tarehe 06 Desemba, 2019 na kumalizika tarehe 12 Desemba, 2019.
Vituo vya Uandikishaji vitakuwa kwenye Mitaa na Vijiji katika Kata zote za Mikoa hiyo na vitafunguliwa kuanzia saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni na uandikishaji utafanyika kwa muda wa siku saba katika kila kituo
Uboreshaji utahusisha :-

  • Kuandikisha Wapiga Kura wapya waliotimiza umri wa Miaka 18 na zaidi na wale watakaotimiza umri huo ifikapo siku ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.
  • Kuandikisha wale wote ambao wana sifa lakini hawakujiandikisha 2015
  • Kutoa kadi mpya kwa wapiga kura waliopoteza kadi zao
  • Kutoa kadi mpya kwa wapiga kura ambao kadi zao zimeharibika
  • Kuhamisha taarifa za wapiga kura waliohama kata au majimbo na kwenda katika maeneo mengine ya kiuchaguzi
  • Kurekebisha taarifa za wapiga kura ambazo zilikosewa mfano majina
  • Kuondoa wapiga kura waliopoteza sifa kama vile waliofariki dunia.

UBORESHAJI WADAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA UTAHUSISHA MAMBO YAFUATAYO:-
Mwananchi anatakiwa kupanga mstari akiwa kituoni.
Watu wenye ulemavu, wajawazito, akina mama wenye watoto, wagonjwa na wazee watapewa kipaumbele.
Kama ulijiandikisha mwaka 2015, taarifa zako ziko sahihi, hujahama eneo lako la uchaguzi, hujapoteza kadi au kadi yako haijaharibika hautahusika na zoezi hili.
Wito unatolewa kwa wale wote wenye sifa za kuandikishwa, kujitokeza katika kipindi hiki cha awamu ya kwanza ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.

KUMBUKA
Sifa muhimu ya kukuwezesha kupiga kura siku ya Uchaguzi Mkuu ni kuwa na kadi ya mpiga kura.

KADI YAKO KURA YAKO, NENDA KAJIANDIKISHE.
Tangazo hili limetolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi, S.L.P. 10923, Dar es Salaam. Tel.+255 22 2114963-6. Nukushi: +255 22 2113382. Barua Pepe: info@nec.go.tz. Tovuti: www.nec.go.tz.

Attachment: Download