MKUTANO WA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI NA WADAU WA UCHAGUZI ULIOFANYIKA MKOANI MOROGORO
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imefanya kikao na wadau wa uchaguzi mjini Morogoro kwa lengo la kupeana taarifa mbalimbali kuhusu zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na maandalizi mengine kuelekea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba mwaka huu.
Mkutano huo uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro umejumuisha viongozi wa vyama siasa, viongozi wa dini, wawakilishi wa wazee wa kimila na wawakilishi wa watu wenye ulemavu. Mkutano huo pia umeshirikisha wawakilishi wa vijana na wanawake, wawakilishi wa asasi za kiraia, wahariri wa vyombo vya habari na waandishi wa habari.
Kwa maelezo zaidi tafadhali pakua taarifa iliyoambatanishwa.