UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM
RESEARCH AND EDUCATION FOR DEMOCRACY IN TANZANIA (REDET)

Announcements

Kwa mujibu wa kifungu cha 4C cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, Tume Ma jukumu la kutoa Elimu ya Mpiga Kura nchi nzima, kuratibu na kusimamia watu wanaotoa elimu hiyo.

 

Kwa mantiki hiyo, Tume ya Taifa ya Uchaguzi inapenda kuzialika Taasisi/ Asasi zenye nia ya kutoa Elimu ya Mpiga Kura kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 kuwasilisha maombi yao Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Mwisho wa kupokea maombi ni Tarehe 20 Januari, 2020.

 

Taasisi/Asasi itayakayowasilisha maombi inatakiwa kukidhi vigezo vifuatavyo:-

  1. Iwe na usajili kwa mujibu wa Sheria za Tanzania.
  2. Iwe imefanya kazi Tanzania si chini ya miezi 6 toka kusajiliwa kwake.
  3. Miongoni mwa Watendaji wake Wakuu watatu, wawili wanapaswa wawe Watanzania.
  4. Iwe haina taarifa za kuvuruga amani au kuchochea fujo ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na katika nchi yoyote.
  5. Iwe tayari kujigharamia katika kutoa Elimu ya Mpiga Kura.

 

Aidha, maombi hayo yanatakiwa kuambatanishwa na:‑

  1. Cheti cha Usajili.
  2. Katiba ya Taasisi /Asasi.
  3. Majina ya Viongozi wa juu wa Taasisi/ Asasi
  4. Anuani kamili ya makazi (Physical Address) na namba za simu za Ofisi na Viongozi.
  5. Ratiba na maeneo wanayotarajia kutoa Elimu ya Mpiga Kura.

 

Tume haitahusika na utolewaji wa fedha za kugharamia shughuli za kutoa Elimu ya Mpiga Kura. Aidha, Tume itafuatilia Taasisi/ Asasi zitakazopewa Kibali cha kutoa Elimu ya Mpiga Kura kwa lengo la kuona kama elimu hiyo inatolewa kwa kufuata taratibu zilizowekwa.

 

Maombi yote yatumwe kwa anuani ifuatayo:-

Mkurugenzi wa Uchaguzi,

Tume ya Taifa ya Uchaguzi,

Jengo la Wizara ya Mambo ya Nje,

Mtaa wa Shaaban Robert/ Garden Avenue,

S. L. P. 10923,

Dar Es Salaam.

Attachment: Download