Announcements

“Badili changamoto kuwa fursa”

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam anawatangazia wahitimu wote wa Vyuo vya Elimu ya Juu Tanzania kuwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kimeandaa mafunzo ya ujasiriamali yatakayotolewa katika mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Arusha, Unguja, Pemba, Kigoma, Kagera, Iringa na Lindi. Mafunzo haya yataanza mwezi Septemba hadi mwezi Oktoba mwaka 2023.

LENGO KUULA MAFUNZO

Kuwapatia vijana uelewa, taarifa, maarifa, ujuzi na uwezo wa kuainisha fursa zinazowazunguka na kuweza kuzitumia fursa hizo kuanzisha ajira/biashara kwa ajili yao na wenzao na hivyo kuboresha maisha ya jamii kwa ujumla.

MALENGO MAHUSUSI

  • Kujenga tabia na uwezo wa kutumia taaluma zao kuona matatizo na changamoto kama fursa.
  • Kukutana na kujifunza kutoka kwa wajasiriamali wazoefu kutoka kwenye sekta mbalimbali kama vile, kilimo, ufugaji, madini, viwanda na huduma.
  • Kutengeneza michanganuo ya mawazo ya kibiashara ambayo itawasaidia kuanzisha na kuendeleza biashara, kutafuta mitaji, na kuwa na utaratibu mzuri wa kutumia mitaji.
  • Kuwaunganisha vijana wenye mawazo mazuri ya ujasiriamali, na ambao tayari wapo katika vikundi vya biashara, na watoa huduma za kifedha, teknolojia, uatamizi, nk

WALENGWA

Mafunzo haya yanawalenga vijana wahitimu wa Vyuo vya Elimu ya Juu kuanzia ngazi ya Diploma na kuendelea wenye nia ya kujiajiri. Pia vikundi vya vijana wajasiriamali waliosajiliwa katika ngazi ya manispaa kwa mikoa ya Lindi, Dar es Salaam na Iringa wanahamasishwa kutuma maombi. Sharti ni kwamba katika vikundi hivyo mwanachama mmoja au zaidi awe ni mhitimu wa chuo cha elimu ya juu.

MUDA WA MAFUNZO

Mafunzo haya yatatolewa katika makundi ya watu wasiozidi 50 kwa darasa, kwa muda wa siku nne mfululizo.

RATIBA YA MAFUNZO

Mahali

Tarehe za Mafunzo

Mwisho wa Kujisajili

Dar es Salaam

25/09- 12/10/2023

01/10/2023

Dodoma

16- 20/10/2023

10/10/2023

Arusha

16- 20/10/2023

10/10/2023

Unguja

16- 20/10/2023

10/10/2023

Pemba

16- 20/10/2023

10/10/2023

Kigoma

16- 20/10/2023

10/10/2023

Kagera

16- 20/10/2023

10/10/2023

Iringa

16- 20/10/2023

10/10/2023

Lindi

16- 20/10/2023

10/10/2023

GHARAMA ZA MAFUNZO

Washiriki hawatalipa ada yeyote ya ushiriki wa mafunzo, ila watajigharamia usafiri na malazi (kama ikilazimu).

JINSI YA KUSHIRIKI

Jisajili kwa kujaza fomu ya maombi mtandaoni kupitia https://udsm-gep.ac.tz/ ukiainisha:

  1. Majina yako na namba ya simu.
  2. Mkoa utakapohudhuria mafunzo.
  3. Ambatanisha nakala ya cheti cha kuhitimu masomo yako ya elimu ya juu.
  4. Na kwa walio katika vikundi kwa Mikoa ya Lindi, Dar es Salaam na Iringa; ambatanisha cheti cha usajili au barua ya uthibitisho toka ofisi ya manispaa husika

Kwa changamoto zozote katika kuwasilisha maombi wasiliana nasi kupitia:

  • Barua pepe kwenye anuani: udiec@udsm.ac.tz
  • WhatsApp no.: +255-734-669-818
  • Au +255 745 015 421; +255 759 156 426 kwa msaada zaidi.

 

“WAHI KUJIANDIKISHA NAFASI NI CHACHE”

Kwa Mawasiliano Zaidi:

Mkurugenzi, Kurugenzi ya Ubunifu na Ujasiriamali,

Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam

S.L.P 110099 Dar es Salaam

Simu: +255-737-828-091

Attachment: Download