Announcements

TAARIFA KWA UMMA

TANZIA

img

Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. William A. L. Anangisye, anasikitika kutangaza kifo cha Daktari Elineema Kennedy Kisanga (1978-2023), kilichotokea tarehe 3 Julai 2023, Dar es Salaam.

Dkt. Kisanga alikuwa Mhadhiri katika Shule Kuu ya Uchumi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Alianza kazi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kama Mkufunzi Msaidizi wa Uchumi mwaka 2006 na kupanda kitaaluma hadi ngazi ya Mhadhiri ambayo alihudumu hadi alipofariki.

Dkt. Kisanga alikuwa mbobevu katika tasnia ya uchumi ambapo alitafiti, kuchapisha na kufundisha shahada za awali na uzamili katika Uchumi Mkuu Uchumi wa Usafirishaji, Uchumi wa Afya na Uchumi wa Fedha za Umma.

Mipango ya mazishi ya Marehemu Kisanga inafanywa na familia ikishirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Ibada na Itifaki ya kuaga itafanyika Ijumaa tarehe 7 Julai 2023 katika Kanisa la KKKT Boko na kisha kusafiri kwenda Moshi, Kilimanjaro kwa Mazishi yatakayofanyika siku ya Jumamosi tarehe 8 Julai 2023.

Roho ya Marehemu Ipumzike kwa Amani!

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano na Masoko 5 Julai 2023

Attachment: Download