Chama cha Hisabati Tanzania (MAT/CHAHITA) kwa kushirikiana na idara ya Hisabati ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam itafanya famunzo endelevu ya wiki moja kwa walimu wa somo la Hisabati. Mafunzo haya yatahusisha walimu wa shule za msingi, sekondari na vyuo vya ualimu vya kati na vyuo vikuu. Hii ni sehemu ya mafunzo endelevu ya walimu kazini. Mafunzo haya yatafanyika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine Morogoro Kampasi ya Solmon Mahlangu (Mazimbu), kuanzia tarehe 29 Agosti mpaka tarehe 3 Septemba 2022.
Walimu na wadau wote wa somo la Hisabati mnakaribishwa. Kwa maelezo zaidi wasiliana na
Katibu mkuu wa MAT/CHAHITA
Simu No. 0713 - 496638 au 0745 - 626665
Barua Pepe: said.sima@gmail.com