Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. William A. L. Anangisye, anasikitika kutangaza kifo cha Dkt. Paul Ochien’g Onyango (1970-2022), kilichotokea tarehe 10 Aprili 2022 katika Hospitali ya Kairuki, Dar es Salaam. Dkt. Onyango alikuwa Mhadhiri Mwandamizi katika Idara ya Sayansi Akua na Teknolojia ya Uvuvi, Shule Kuu ya Sayansi Akua na Teknolojia ya Uvuvi. Alianza kazi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kama Mhadhiri Msaidizi mwaka 2007. Alipanda vyeo vya kitaaluma hadi kufikia ngazi ya Mhadhiri Mwandamizi mwaka 2016.