Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. William A. L. Anangisye, anasikitika kutangaza kifo cha Bi. Zainabu Hassan Maro kilichotokea tarehe 27 Machi 2023 katika Hospitali ya Hubert Kairuki Dar es Salaam. Marehemu Bi. Zainabu Hassan Maro alikuwa Afisa Mkutubi Mwandamizi katika Maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.