Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. William A. L. Anangisye, anasikitika kutangaza kifo cha Prof. Matthew Laban Luhanga (1948-2021), kilichotokea tarehe 16 Septemba 2021 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. Marehemu Prof. Luhanga alikuwa Profesa katika Idara ya Uhandisi Elektroniki na Mawasilianopepe, Ndaki ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (CoICT). Aliajiriwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa wadhifa wa Mhadhiri mwaka 1976. Alipandishwa vyeo vya kitaaluma hadi kufikia ngazi ya Profesa. Prof. Luhanga alistaafu rasmi utumishi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 2018.

SOMA ZAIDI >>>