TAKWIMU POTOFU KUHUSU WANAFUNZI WA UDSM

Kuna taarifa inayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu takwimu za wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na wa vyuo vingine vya umma hapa nchini kuhusiana na maambukizi ya VVU. Tunaujulisha umma kuwa taarifa hiyo haina ukweli wowote.

Tunalaani uzushi huu uliolenga kuichafua taswira ya UDSM kwa maslahi binafsi.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano na Masoko
10 Novemba 2023

 

Attachment: 20231110_071935_UDSM_TAARIFA KWA UMMA....pdf