Ofisi ya Makamu Mkuu wa Chuo Mipango Fedha na Utawala, inawafahamisha wasailiwa waliofanya usaili wa vitendo na kuchaguliwa kuendelea na usaili wa mahojiano kuwa usaili utafanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kama ifuatavyo;-
TAREHE YA USAILI : 8 DESEMBA 2023
MUDA : KUANZIA SAA MBILI NA NUSU (2:30)ASUBUHI
UKUMBI : COSS BOARD ROOM

Wasailiwa wote wanapaswa kuzingatia mambo yafuatayo:-
i. Kuwasilisha vyeti halisi kuanzia cheti cha kuzaliwa, cheti cha kidato cha nne, cheti cha udereva na Leseni ya udereva,;
ii. Kitambulisho cha Taifa (NIDA), Mpiga Kura, Pasi ya Kusafiria au barua ya utambulisho kutoka serikali ya mtaa kwa ajili ya utambuzi;
iii. Wasailiwa watakaowasilisha “Provisional Results”, “Statement of Results”, hati za matokeo ya kidato cha IV na VI (Form IV and VI results slips) HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI;
iv. Kila msailiwa azingatie tarehe, muda, na mahali ambapo usaili utafanyika;
v. Kila msailiwa atajigharamia chakula, usafiri na malazi;

Read More >>>