Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kinapenda kuwataarifu na kuwaalika wadau na Watanzania wote kwa ujumla kushiriki katika Maadhimisho ya Saba ya Wiki ya Utafiti na Ubunifu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yatakayoanza Jumanne tarehe 24 Mei hadi Alhamisi tarehe 26 Mei 2022 kuanzia saa 2:00 asubuhi mpaka saa 10:00 jioni katika eneo la Maktaba Mpya, Kampasi ya Mwalimu Julius Nyerere, Mlimani. Ufunguzi rasmi wa Maadhimisho haya utafanyika siku ya Jumanne tarehe 24 Mei 2022 katika Ukumbi wa Maktaba kuanzia saa 2.00 asubuhi, ambapo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kaulimbiu ya Maadhimisho haya ya Saba ya Wiki ya Utafiti na Ubunifu ni Utafiti na Ubunifu kwa Manufaa ya Kijamii Nchini Tanzania

SOMA ZAIDI >>>