Uzinduzi Rasmi wa Shahada ya Uzamili ya Haki Miliki CKD

Thu, 01.Jan.1970 03.00

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kushirikiana na Wakala wa Usajili na Uhuishaji wa Biashara (BRELA) na Shirika la Haki Miliki la Afrika (ARIPO) kimezindua rasmi Shahada ya Uzamili ya Haki Miliki. Uzinduzi huo umeambatana na kusaini makubaliano ya awali juu ya ubadilishanaji wa wataalamu, kujenga uwezo na ufadhili kwa baadhi ya wanafunzi katika programu hiyo.