UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM
DAR ES SALAAM UNIVERSITY COLLEGE OF EDUCATION (DUCE)

News

Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu (DUCE) kimezindua rasmi jengo maalum la huduma ya Afya ya Uzazi na Mtoto (Reproductive and Child Health – RCH). 

Jengo hilo lipo katika Zahanati ya Chuo ambapo kuna vyumba vinne vya madaktari na vifaa maalum vya kutolea huduma ya Afya ya Uzazi na Mtoto.

Akiongea kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Bi. Aimbora Nnko, alikipongeza Chuo kwa kuunga mkono juhudi za serikali ya Raisi Dkt. John Pombe Magufuli kuboresha huduma za afya kwa jamii.

‘Raisi wetu Dkt. John Pombe Magufuli anafarijika anapoona taasisi za serikali zinaunga mkono juhudi zake, na jengo hili ni kielelezo halisi,’ alisema Bi. Nnko akiwasilisha salamu kutoka kwa Mkuu wa Wilaya Bw. Felix Lyaniva.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu (DUCE), Prof. Bernadeta Killian, alisema jengo hilo limejengwa kwa kutumia mapato ya ndani ya Chuo akipongeza serikali kwa kuendelea kusaidia juhudi za Chuo kuboresha hali ya utoaji taaluma na huduma kwa jamii kwa ujumla, kama yalivyo malengo ya Kuanzishwa kwa Chuo hiki.