Rasi wa Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE), Prof. Stephen Oswald Maluka, anasikitika kutangaza kifo cha Mtumishi wa Chuo, Bi. Nora Michael Ngirwamungu {Afisa Tawala Mkuu II} kilichotokea tarehe 14/07/2021 baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Taratibu za mazishi zinafanyika nyumbani kwake Chang ' ombe, karibu na uwanja wa Sigara.
Tunatoa pole kwa wote walioguswa na msiba huu.