UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM
DAR ES SALAAM UNIVERSITY COLLEGE OF EDUCATION (DUCE)

Announcements

Naibu Rasi (Mipango, Fedha na Utawala) wa Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) anapenda kuwataarifu Waombaji Kazi waliofanyiwa usaili wa maandishi tarehe 14/09/2022 katika kumbi zilizopo DUCE kuwa usaili wa mahojiano utafanyika kuanzia tarehe16 Septemba, 2022 hadi 19 Septemba, 2022. 

Wasailiwa waliofaulu kuingia kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:

  1. Usaili utafanyika 16 Septemba, 2022 hadi 19 Septemba, 2022 kama ilivyooneshwa kwenye tangazo hili;
  2. Usaili utafanyika katika kumbi za Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam kuanzia Saa moja na nusu asubuhi.
  3. Kila Msailiwa anatakiwa kufika kwenye eneo la usaili akiwa amevaa
    barakoa (mask);
  4. Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi. Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na: Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpiga kura, Kitambulisho cha kazi, Kitambulisho cha Uraia au Hati ya kusafiria.
  5. Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha kuzaliwa, kidato cha IV, VI, Digrii na kuendelea kutegemeana na sifa za Mwombaji.

Orodha ya Wasailiwa imeambatanishwa, tafadhali PAKUA KIAMBATISHO.

Attachment: Download